The House of Favourite Newspapers

Rais Duterte Atangaza Kustaaafu Siasa

0

RAIS Rodrigo wa Ufilipino,  Duterte (76) amesema anajiuzulu siasa na hatagombea katika uchaguzi wa mwakani (2022) katiba ya nchi hiyo inawaruhusu marais kuhudumu muhula mmoja wa miaka sita.

 

Lakini kwa sasa anasema ameamua kujiondoa kwenye kwenye uchaguzi wa mwakani kwani “hisia za Wafilipino wengi ni kwamba hafai kuongoza tena.

 

Hatua hii inakuja huku kukiwa na uvumi kwamba binti yake anaweza kugombea urais binti yake  Sara Duterte-Carpio, ambaye kwa sasa ni meya wa mji wa kusini mwa nchi hiyo wa Davao.

 

Duterte, ambaye anaonekana kuwa mtata “mwenye nguvu “, aliingia madarakani mwaka 2016 ambapo aliahidi kupunguza uhalifu na kutatua mzozo wa madawa ya kulevya nchini humo.

 

Lakini wakosoaji wanasema katika kipindi cha miaka mitano akiwa maadarakani  Duterte amewachochea polisi kufanya mauaji ya ukiukaji wa sheria ya washukiwa katika kile alichokiita “vita dhidi ya madawa ya kulevya ”

Leave A Reply