The House of Favourite Newspapers

Rais Joe Biden Akutana na Viongozi wa Mataifa ya Kiarabu Jeddah Saudi Arabia

0

RAIS wa Marekani Joe Biden leo anatakuna na viongozi wa mataifa ya kiarabu kwenye mji wa mwambao wa Jeddah nchini Saudi Arabia katika kilele cha ziara yake ya siku nne iliyolenga kuimarisha nafasi ya Marekani kwenye kanda ya Mashariki ya Kati na ulimwengu wa kiarabu.

 

Duru kutoka nchini Saudi Arabia zinasema Biden atakuwa na mazungumzo na viongozi wa mataifa sita ya Ghuba pamoja na Misri, Jordan na Iraq na atautumia mkutano huo kutangaza mwelekeo wa sera ya Marekani kwenye eneo la Mashariki ya Kati.

 

Mkutano huo unafanyika siku moja baada ya Biden kuongoza juhudi za kurekebisha mahusiano kati ya Israel na Saudi Arabia pamoja na kujaribu kurejesha ushirikiano uliotetereka kati yake na watawala wa Saudi Arabia Biden aliyewasili Saudi Arabia jana jioni baada ya kuitembelea Israel na eneo la Ukingo wa Magharibi, alifanya mazungumzo na mwanamfalme Mohammed bin Salman yaliyojikita juu ya masuala ya nishati, usalama na kitisho cha Iran.

Leave A Reply