The House of Favourite Newspapers

Rais JPM Atengua Uteuzi wa Waziri Kitwanga Kisa Ulevi

0

kitwanga

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.

Rais Dk. John Magufuli Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kuanzia leo baada ya kuingia bungeni kujibu swali akiwa amelewa.

JPM

Mfahamu Kitwanga

Charles Muhangwa Kitwanga ni Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Awamu ya Tano, ameteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Pombe Magufuli. Yeye ni mbunge wa Jimbo la Misungwi, mkoani Mwanza tangu mwaka 2010 hadi sasa. Kitwanga alizaliwa Septemba 27, 1960 mkoani Mwanza.

 ELIMU

Kitwanga amepata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Busagara mkoani Mwanza kati ya mwaka 1970 hadi 1976 na elimu ya sekondari kwa kidato cha kwanza hadi cha nne katika Shule ya Sekondari Same mkoani Kilimanjaro kuanzia mwaka 1977 hadi 1980. Kisha kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Tosamaganga mkoani Iringa, kati ya mwaka 1981 hadi 1983.

Kitwanga aliendelea na taaluma ya juu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aliingia mwaka 1985 akichukua Shahada ya Sayansi, akahitimu mwaka 1988. Miaka miwili baadaye, yaani mwaka 1990 alikwenda nchini Uingerea katika Chuo Kikuu cha Essex na kusomea Shahada ya Sayansi ya Umahiri (Uzamili) na kuhitimu akibobea kwenye masuala ya Teknolojia ya Habari (IT), mwaka 1990 hadi 1991.

WAZIRI KITWANGA APOFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA WAKUU WA JESHI LA POLISI BAADA YA KUTEULIWA KUSHIKA WADHIFA HUO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Polisi nchini kabla ya kufungua kikao kazi chaJeshi la polisi katika  Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akitoa hotuba yake kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) kuzungumza na maafisa hao kutoka mikoa yote nchini na kuufungua kikao kazi  kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB nchini, Ineke Bussemaker, mara baada ya kumkabidhi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia), Shilingi Milioni 75 kwa ajili ya kuudhamini kikao kazi   cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa yote nchini.

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, wakimsikiliza mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alipokuwa anazungumza na maafisa hao katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.

UZOEFU

Kitwanga alianza kupata uzoefu wa kazi mara alipohitimu kidato cha sita kwani aliajiriwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Kauma akiwa Ofisa Usafirishaji Msaidizi na kufanya kazi hiyo kati ya mwaka 1984 hadi 1985.

Ajira yake ya kwanza iliyotokana na ubobezi wake kwenye masuala ya IT ilikuwa ni Benki Kuu ya Tanzania (BoT), aliajiriwa mwaka 1988 akafanya kazi hadi 1992 katika nafasi ya Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari.

Kuanzia mwaka 1992 hadi 1998 akiwa hapo BoT, alihamishiwa kitengo cha utawala na kufanya kazi kama Ofisa Utawala wa Benki. Alihudumu katika nafasi hiyo kwa miaka 12 mfululizo, kuanzia mwaka 1998 hadi 2010, alipopandishwa cheo na kufanya kazi akiwa Naibu Mkurugenzi wa benki hiyo, akijihusisha na eneo la Uundaji wa Mifumo na Utawala.

Mwaka 2010, Kitwanga aliamua kujitosa kwenye kura za maoni ndani ya CCM ili kuwania ubunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza. Kwenye kura za maoni, alifanikiwa kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo na mtu aliyekuwa akitetea nafasi yake, Jacob Shibiliti pamoja na mshindani mwingine wa karibu, Madoshi Makene.

Mwaka huo wa 2010, Kitwanga au kwa jina la utani ‘Mawe Matatu’, aliingia kwenye uchaguzi wa jumla na kuiweka juu CCM kwa kupigiwa kura 41,935 sawa na asilimia 83.24 huku mshindani wake kutoka Chadema, Jane Kajoki akipata kura 5,293 sawa na asilimia 10.51 na Abdallah Mtina wa CUF alipata asilimia tatu ya kura zote.

Miaka mitano ya mwanzo ya ubunge wa Kitwanga (2010– 2015), ilifuata kwa kumuweka juu katika siasa za Tanzania. Rais Jakaya Kikwete wakati huo, akamteua kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, kuanzia Novemba 2010 hadi Machi 2012, kisha akahamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais na kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais kuanzia mwezi huo hadi Januari 2014 na kuanzia Januari 2014 hadi Novemba 2015, amekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini.

Agosti mwaka 2015, Kitwanga alishiriki kwa mara nyingine kura za maoni ndani ya CCM ili atetee kiti chake cha ubunge wa Misungwi ambako akashindana na kumshinda hasimu wake kisiasa, mbunge wa zamani wa Misungwi, Jacob Shibiliti. Kitwanga alipigiwa kura 26,171 sawa na asilimia 69.9 huku Shibiliti akipata kura 7,009 sawa na asilimia 18.

Kwenye uchaguzi wa jumla uliofanyika Oktoba 25, 2015 Kitwanga alishinda tena kwa kupigiwa kura 72,072 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Leonidas Kandela wa Chadema, aliyepigiwa kura 18,050 na kuwa wa pili.

Baada ya ushindi wake wa ubunge wa mara ya pili, ndipo Rais JPM akamkabidhi Kitwanga Wizara ya Mambo ya Ndani akawa waziri, akichukua mikoba ya Mathias Chikawe, aliyehudumu kwenye wizara hiyo nyakati za mwisho za Rais Kikwete.

Ndani ya CCM, Kitwanga amekuwa na uzoefu wa muda mrefu. Kwanza amekuwa mlezi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), wilayani Misungwi kuanzia mwaka 2006, halafu akawa mjumbe wa Baraza la Wilaya la CCM mwaka 2008, kisha akateuliwa kuwa Kamanda wa UVCCM wa Mkoa wa Mwanza mwaka 2009.

Wanasiasa wanazungumziaje hili la Kitwanga

 Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa facebook kuandika mtazamo wake baada ya Rais Magufuli kufanya maamuzi hayo ya kumfuta kazi waziri Kitwanga.

“Uamuzi wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja – hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata aliowateua. Ni maamuzi muhimu sana kwa Kiongozi wa aina yake. Wale vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha Uongozi ‘ no nonsense “


Haya ni maneno ya Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Mhe. Godbless Lema

Video ya Lema alichokizungumza Bungeni siku 3 kabla ya Kitwanga kutumbuliwa

TAZAMA VIDEO YA WAZIRI KITWANGA AKIJIBU SWALI BUNGENI HUKU AMELEWA

 

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply