The House of Favourite Newspapers

Rais Kenyatta Aondoa ‘Lockdown’ Kenya

0
 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta  ametangaza kuondoa zuio la watu kutotoka nje katika kaunti tano nchini humo kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya corona.

Ameyasema hayo leo Mei 01, 2021 katika maadhimisho ya  kusheherekea siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) Nairobi.

 

Katika taarifa yake rais Kenyatta  wakati alipotoa agizo la pili kwa umma mnamo Machi 2021, la jinsi ya kukabiliana na janga la Corona, Nairobi ilikuwa na maambukizi 56,815.

 

Maambukizi yalipungua mwezi Aprili kwa chini ya 15,000, hii ikionesha asilimia 74% ya maambukizi yamepungua mjini Nairobi.

 

Takwimu za wataalamu wetu wa afya zinaonesha hali kama hiyo katika eneo ambalo tuliweka katazo la watu kutotoka nje mwezi Machi 26, 2021.

 

Baada ya mwezi mmoja wa marufuku ya kutoka nje , kesi za maambukizi ya COVID yamepungua mpaka 72%.

Maeneo mengine ya nchi , maambukizi ya COVID yamepungua kwa 89% Mombasa na 90% Busia kati ya mwezi Machi na Aprili 2021.

Leave A Reply