The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Aahidi Kulipa Bilioni 200 Madeni Ya Ndani Kuanzia Mwezi Ujao (Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kuwa wezi ujao serikali itaanza kulipa madeni ya ndani yatakayokuwa yamehakikiwa.

 

Rais Magufuli ameyasema hayo Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo baada ya kuagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake, Prof. Benno Ndulu na kueleza kuwa, mwezi ujao Serikali itatoa Shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya kulipa madeni ya ndani yatakayokuwa yamehakikiwa, yakiwemo ya wazabuni mbalimbali waliotoa huduma katika taasisi za Serikali, madai ya walimu na madai ya wakandarasi.

 

“Nasisitiza madeni tutakayolipa ni ya ndani, na tutalipa madeni ambayo yamehakikiwa, kwa hiyo maandalizi ya kutoa fedha hizo yaanze mara moja na ni matarajio yangu fedha hizi zitasaidia kuchochea ukuaji wa uchumi wetu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Bofya hapa kutazama video

Comments are closed.