Rais Museveni Ampandisha Cheo Tena Mwanaye Jeshini

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amempandisha cheo mwanaye, Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mmoja ya maafisa waandamizi wa Jeshi kutoka cheo cha Meja Jenerali hadi Luteni Jenerali ambacho ni cheo cha tatu kwa ukubwa kwenye jeshi la nchi hiyo baada ya Jenerali & Field Marshal.

 

Utakumbuka Mei 2016, Rais Museveni alimpandisha cheo mwanaye huyo na kufikia ngazi ya Meja Jenerali ambaye anatambulika kama mtu mwenye nguvu sana katika jeshi la nchi hiyo.

 

Wengi wanaamini kuwa anatengenezwa kwa ajili ya kumrithi baba yake kitu ambacho wamekuwa wakikipinga vikali.Hata hivyo kwa upande mwingine, Muhoozi amewahi kuweka wazi malengo yake ya kuwa mwanasiasa.

 

Inaelezwa kuwa, katika mfumo wa majeshi duniani, Luteni Jenerali ndiye Commissioned officer mwenye cheo na madaraka ya juu zaidi jeshini baada ya Mkuu wa Majeshi (Jenerali). Kwa Tanzania Luteni Jenerali hupewa madaraka ya kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi. Na ikitokea Mkuu wa Majeshi amestaafu, Luteni Jenerali atapandishwa kuwa Jenerali na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi.

 

Kwa mfano, Jenerali Mabeyo alikua Luteni Jenerali wakati Jenerali Mwamunyange akiwa Mkuu wa Majeshi. Jenerali Mwamunyange alipostaafu, Mabeyo alipandishwa kuwa Jenerali kamili na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi. Hata Mwamunyange naye alikuwa Luteni Jenerali wakati Jenerali Waitara akiwa Mkuu wa Majeshi. Waitara alipostaafu, Mwamunyange alipandishwa kuwa Jenerali.

 

Mkuu wa majeshi nchini Uganda, Jenerali Edward Katumba Wamala (mwenye umri wa miaka 65) alipaswa kustaafu tangu mwaka 2017. Lakini Rais Meseveni akamuongezea mkataba.

Loading...

Toa comment