
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kuanzia Agosti 18, 2021.
Katika taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Abdul Mohamed inaeleza kuwa pia Rais Mwinyi amemteua Balozi Amina Salum Ali, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Takwimu Zanzibar kuanzia Agosti 16, 2021.
Katika uteuzi mwingine, Rais Dk. Mwinyi amemteua Salma Haji Saadat kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu na Ussy Khamis Dede kuwa Mkurugenzi wa baraza hilo, uteuzi ulioanza Agosti 18, 2021.


