Rais Samia Atoa Rai kwa Wizara ya Kilimo Kuanzisha Kilimo cha Kisasa (Picha +Video)
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Wizara ya Kilimo kuanzisha na kuendeleza kilimo na ufugaji wa kisasa ikiwa ni sambamba na kuweka mikakati ya ujenzi wa viwanda vidogovidogo hasa katika mikoa ya Tabora na Katavi.
Rais Samia ameyasema hayo wakati anafungua Barabara ya Tabora- Koga-Mpanda yenye urefu wa Kilomita 342.9 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Rais Samia amesisitiza kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo utawezesha kukua kwa uchumi wa mikoa husika lakini pia taifa kwa ujumla na itasaidia zaidi katika upatikanaji wa mazao yanayozalishwa kutoka mashambani ambayo kwa kiwango kikubwa mikoa hiyo imekuwa ikijitahidi katika uzalishaji.
Rais Samia pia amegusia kuwa barabara hiyo imejengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa gharama ya shilingi Bilioni 473.879