The House of Favourite Newspapers

Rammy apata shavu Ghana

0

Rammy Galis

Stori: Boniphace Ngumije

MUUZA sura kwenye filamu za Bongo, Rammy Galis ‘Pacha wa Kanumba’ amezidi kula mashavu katika Tasnia ya Filamu Ghana na hivi karibuni anatarajiwa kudandia pipa kuelekea nchini humo kwa ajili ya kugonga filamu nyingine na dairekta maarufu nchini humo anayejulikana Afrika nzima.

Akichonga na gazeti hili Rammy Galis alisema filamu alizofanya na wasanii kutoka Ghana na Nigeria ambazo ni Red Frag, Her Shoes na Cris Cross ndizo zimemfanya kupata jina zaidi Afrika Magharibi hata kuendelea kupata mashavu hayo lakini pia yuko katika maongezi mazuri na prodyuza Sylivester Madu ‘Rambo wa Nollwood’ aliyekwishafanya naye kazi awali ili wapige mzigo tena.

“Kwa sasa filamu ninayokwenda kucheza Ghana ni sapraizi lakini wapenzi wa kazi zangu watarajie kitu kikubwa sana na wasanii maarufu kutoka huko na kazi ikiwa tayari nitawaeleza. Kikubwa ninaomba wapenzi wa filamu wanisapoti maana kwa sasa mimi ndiye Mtanzania pekee ninaye komaa kwenda nje,” alisema Rammy Galis.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply