The House of Favourite Newspapers

Raphinha Aitosa Chelsea Akaribia Kujiunga na Barcelona, Leeds United Yakubali Ofa ya Barca

0
Raphinha winga wa Leeds United na Timu ya Taifa ya Brazil

WINGA wa klabu ya Leeds United ya Uingereza raia wa Brazil Raphinha anakaribia kujiunga na klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispoania kwa ada ya zaidi ya Paundi Milioni 70.

 

Raphinha mwenye umri wa miaka 25 amekuwa kwenye rada za vigogo hao wa soka Duniani huku pia akiwaniwa kwa karibu na klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza.

 

Chelsea ndiyo ilikuwa klabu ya kwanza kkubaliana ada ya uhamisho na Leeds United kwa ajili ya uhamisho wa nyota huyo lakini Raphinha alisubiri ofa ya Barcelona kwani kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya vimebainisha kuwa Raphinha amekuwa na ndoto ya kuichezea klabu ya Barcelona tangu akiwa mdogo.

Raphinha ameitosa Chelsea na kujiunga na Barcelona

Wakala wa mchezaji huyo ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona na Chelsea Deco De Souza ndiye anayesimamia kwa karibu sakata la uhamisho wa mchezaji huyo anayegombewa na vilabu hivyo viwili ambapo kwa sasa Barcelona wanaonekana kuwa na asilimia kubwa ya kuinasa saini ya mchezaji huyo.

Leave A Reply