The House of Favourite Newspapers

RASMI KOCHA MPYA WA SIMBA HUYU HAPA, WENYEWE WAMTANGAZA

Kocha  Mkuu mpya wa Simba Mfaransa Pierre Lechantre.

Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya, Mfaransa Pierre Lechantre.

Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo

Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.

Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.

Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi

Na leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa.

IMETOLEWA NA

HAJI S MANARA

MKUU WA HABARI SIMBA SC

 

SIMBA SC NGUVU MOJ

Comments are closed.