The House of Favourite Newspapers

RASMI: TIGO FIESTA 2018 DAR ES SALAAM KUFANYIKA WIKI IJAYO

Uongozi wa Clouds Media Group umetangaza upya tarehe na sehemu itakayofanyika Tasmasha la Tigo Fiesta kabla ya mwaka mpya baada ya mara ya kwanza kuahirishwa katika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam.

 

Ikumbukwe kwamba Fiesta ilifanyika karibia mikoa 15 nchini Tanzania lakini ilipofika wakati wa kufanyika hapa Dar Es Salaam ambayo ndio ilikuwa inafunga msimu mpya wa Fiesta ilisitishwa kwa madai kwamba sehemu ambako ingeenda kufanyika ingeleta taharuki kutokana na kelele zitakazojitokeza mahala hapo.

 

Uongozi wa CGM umetangaza kupitia kurasa zao za kijamii tarehe mpya na sehemu ambako Tamasha hilo litafanyika

 

“Tarehe 22 Desemba kwenye Viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam, Machampion wote wa nchi wanakwenda kutoa shukrani moja kubwa na kushangalia mafanikio ya mwaka huu. Ni mara 2 ya tulichokimiss: stage ya viwango, sound kubwa kuliko, bata la kihistoria na list ndefu ya machampion. . #TigoFiesta2018, ” imeandika Clouds Media.

BREAKING: Rais Magufuli Akihutubia wakati Akitia Saini Mradi wa Stiglers Gorge

Comments are closed.