The House of Favourite Newspapers

RAYVANNY: MGAHAWA WA JUISI ULINIFANYA NIMPATE FAYMA

Image result for rayvanny na rayvanny

MPENZI msomaji tunazidi kutiririka katika safu yetu hii yenye kuvutia, ambapo wiki iliyopita tulikuwa na mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Kherry Sameer maarufu kama Mr. Blue akisimulia namna ambavyo alivyowezakukutana na kipenzi chake, mama wa watoto wake Wahida, mpaka wakaamua kufunga ndoa na leo tunakuwa na Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ pamoja na mama wa mtoto wake Fahyma, akielezea walivyokutana.

 

Tembea naye…

NAKUMBUKA nilikutana na kipenzi changu sehemu moja hivi maeneo ya Kinondoni, alikuwa anapenda kwenda kupata juisi pale. Mara nyingi alikuwa akienda, ikabidi nianze kumfuatilia kwa kuwa mimi nilipenda kuishi naye na kujenga familia.

 

Nikawa nakwenda pale ili niweze angalau kuongea naye. Siku moja alikuja kama kawaida yake, ikabidi nimfuate ili niweze kumuomba namba ya simu na hivi nilikuwa natambulika tayari, alishangaa sana.

 

Mawasiliano yaliendelea hatimaye tukajenga mazoea. Nikaamua kumueleza ukweli wangu, haikuwa rahisi kwa sababu si unajua mtoto wa kike hawezi kuamini mara moja kama kweli unampenda kwa dhati, ilichukua muda kidogo kukubaliana na mimi.

Image result for rayvanny na fayvanny

Baada ya muda alikubali tukaanza maisha, japokuwa kulikuwa na changamoto nyingi na kuna kipindi tulizushiwa kuwa hatupo pamoja lakini kama Mungu ameamua kupanga muwe pamoja, hakuna anayezuia.

 

Tumebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume Jayden na tulijaliwa kwenda kumbatiza nyumbani kwetu Mbeya na Fayma aliingia kanisani kwa ajili hiyo.

 

Nilikwenda kumtambulisha nyumbani na wazazi wakaridhia, mpaka sasa tupo pamoja na ninampenda sana na naomba Mwenyezi Mungu atujaalie, tuendelee kuishi kwa amani na upendo wa dhati asisikilize maneno ya watu.

MUHIMU: Kwa mwenye simulizi yake tamu na namna alivyokutana na mpenzi wake, bila kujali ustaa, anaweza kutuma picha ya harusi yake na maelezo kwenye namba: 0718-008 152.

Msimuliaji: Raymond Mwakyusa Mwandishi: Neema Adrian

Comments are closed.