The House of Favourite Newspapers

Meya, DED Kinondoni Wamaliza Mgogoro

0

MKUU wa mkoa wa Dar es salaam,  Amos Makalla amemaliza sintofahamu ya uongozi wa manispaa ilijitokeza kati ya meya manispaa ya Kinondoni,  Songoro Mnyonge na mkurugenzi wa manispaa Spora Liana.

Usuluhishi wa mgogoro huo umefanyika leo Mei 21, 2021 katika kikao cha pamoja kilichoitishwa leo na mkuu wa mkoa na kuwakutanisha meya na mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni.

Mkuu wa mkoa amewataka viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

Kwa upande wa Meya na mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya wananchi.

 

Leave A Reply