The House of Favourite Newspapers

RC Makonda: “Mdee, Msigwa Ole Wenu Mtukane” – Video

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda amezindua mabweni ya wanafunzi katika Shule ya Mtakatifu Joseph inayomilikiwa na Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kuwataka wazazi kuwalea watoto katika msingi wa neno la Mungu ili kuwaepusha na changamoto za utandawazi.

 

Makonda ameeleza adhma ya serikali kutambua mchango wa kiongozi wa Kanisa Katoloiki nchini, Muhadhama Kadinali Policarp Pengo, ambapo ameagiza moja kati ya barabara kubwa za kisasa mpya zinazojengwa jijini DSM kupewa jina la Kiongozi huyo ili kuenzi mchango wake katika Taifa.

 

Akiongea katika hafla hiyo, Kadinali Pengo amewamshukuru wadau mbalimbali kwa michango yao kufanikisha ujenzi wa mabweni na kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa uamuzi wa kutumia jina lake katika mojawapo ya barabara jijini Dar.

 

Makonda amewaonya wabunge wa Chadema, Halima Mdee na Peter Msigwa kuwa endapo watawatukana viongozi wa dini badi atakula nao sahani moja ikiwa ni kuwakamata na kuwasweka ndani.

VIDEO: MSIKIE MAKONDA AKIFUNGUKA

Comments are closed.