The House of Favourite Newspapers

RC Makonda Kupima Tezi Dume Nyumba kwa Nyumba

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salam, Paul Makonda anatarajia kuanza Oparesheni maalum wa kupima tezi dume kwa lazima nyumba kwa nyumba mkoani Dar es Salaam.

 

Makonda ametoa taarifa hiyo wakati akizindua warsha ya utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana, ikihusisha waandishi wa habari, wataalamu wa afya, viongozi wa dini na siasa ambapo amesema wakati saratani ya mlango wa kizazi ikiwaathiri wanawake nchini, tezi dume inaumiza zaidi akina baba, lakini hakuna mwamko wa kulizungumzia suala hilo.

“Kuna kasumba ya kwamba, saratani ya tezi dume inapimwa kwa kidole, jamani siyo kweli, kuna kipimo cha damu na ni rahisi, hivyo nina mkakati maalum wa kupita nyumba kwa nyumba katika mkoa wangu wa Dar es Salaam ili kuhakikisha hii kasi ya vifo vya akina baba kwa tatizo la tezi dume vinapungua kwa kuwabaini na kuwaanzishia matibabu mapema, ” alisema Makonda.

 

Aidha, Makonda amewataka viongozi wote wa Serikali za Mitaa na viongozi wa dini kutoa elimu kwa jamii ili wasichana wote wafike kwenye vituo vya afya vinavyotoa chanjo hiyo kwa wingi kupata chanjo.

Comments are closed.