The House of Favourite Newspapers

Ripoti ya Pluijm yaishtua Yanga

0

pluijm1

Kocha Mkuu wa Yanga, Mdachi, Hans van Der Pluijm.

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam

JUZI Jumatatu Kocha Mkuu wa Yanga, Mdachi, Hans van Der Pluijm aliukabidhi uongozi wa timu hiyo ripoti yake ya mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana iliyofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ripoti hiyo imedaiwa kuushtua uongozi wa timu hiyo kutokana na mambo mbalimbali ambayo kocha huyo ameyaainisha ndani yake yanayohusiana na mechi hiyo ambayo Yanga ilitoka sare ya bao 1-1.

Moja ya mambo makubwa yaliyoushitua uongozi wa timu hiyo ni jinsi kocha huyo alivyosema kuwa wachezaji wake waliachana na maagizo yake na kuamua kucheza wanavyojua wao.

“Ukiacha hilo, ameainisha pia na mambo mengine ambayo kimsingi siyo vizuri kuyasema lakini kwa namna moja ama nyingine uongozi utakuwa umeyaona na utayafanyia kazi. Kwa kifupi siyo ripoti nzuri,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit alisema: “Ni kweli ripoti hiyo tumeshaipokea na kocha ameainisha mambo mengi lakini siyo vizuri kuyaweka wazi, la msingi ninaloweza kusema ni kwamba tutaifanyia kazi ipasavyo.

“Lengo letu ni kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zilizobaki hivyo tunamshukuru kocha kwa ripoti yake hiyo na sisi kama uongozi tutayafanyia kazi yote yanayotuhusu.”

Leave A Reply