The House of Favourite Newspapers

Ronaldo Aahidi Kuanika Mbivu na Mbichi Hatma Yake Ndani ya Manchester United

0
Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo

NYOTA wa klabu kongwe ya soka ya Manchester United Cristiano Ronaldo ameonesha kuto kukubaliana na kutopendezwa na habari za uongo zinazosemwa dhidi yake kwenye sakata linaloendelea la yeye kusemekana kuwa anashinikiza kuondoka katika klabu hiyo.

 

Klabu ya Manchester United iliyoanza vibaya katika michezo yake miwili ya mwanzo ya ligi kuu ya Uingereza msimu huu, tangu awali iliweka wazi kuwa haina mpango kabisa wa kuachana na Cristiano msimu huu licha ya shinikizo kutoka kwa mchezaji huyo baada ya klabu hiyo kukosa nafasi ya kushiriki mashindano ya klabu bingwa msimu huu.

Cristiano Ronaldo anahusishwa na kushinikiza kuondoka ndani ya klabu yake ya Manchester United

Ronaldo akijibu comment ya shabiki wake kwenye mtandao wa Instagram alisema ndani ya wiki zisizozidi mbili ataongea na waandishi wa habari kuweka wazi kwa kile kinachoendelea baina yake na klabu yake. Akisisitiza kuwa mengi yanayoandikwa na vyombo vya habari si ya kweli juu ya sakata lake hilo.

 

Ronaldo alinukuliwa akisema:

“Watajua ukweli nitakapoongea na waandishi wiki chache zijazo. Vyombo vya habari vinasema uongo. Kwenye daftari langu la kumbukumbu miezi michache iliyopita naona kwenye habari 100 zilizoandikwa, 5 tu zilikuwa sahihi. Fikiria jinsi ilivyo.”

 

Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply