The House of Favourite Newspapers

RPC Kakamba wa Singida Alivyoagwa Dar

rpc-kakamba-1

Mwili ukiingizwa kanisani.

rpc-kakamba-2

Kutoka kushoto ni Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar, CP Simon Sirro, IGP Mstaafu, Said Mwema na IGP Ernest Mangu.

rpc-kakamba-3

Marehemu enzi za uhai wake.

rpc-kakamba-4

Padri akiuombea baraka za mwisho mwili wa Peter Kakamba.

rpc-kakamba-5

IGP Ernest Mangu akitoa heshima za mwisho.

rpc-kakamba-6

Kamanda Sirro akimsalia marehemu.

rpc-kakamba-7

RPC wa Temeke, Gilles Muloto, akipita mbele ya mwili wa marehemu. Anayemfuatia ni RPC wa Kinondoni, Suzan Kaganda.

rpc-kakamba-8

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimbo na RPC wa Ilala, Salum Hamduni, wakipita mbele ya jeneza.

rpc-kakamba-9

RPC wa Ilala, Salum Hamduni akitoa heshima za mwisho.

rpc-kakamba-10

Ndugu wakiaga.

rpc-kakamba-11

Maofisa wa polisi wakiupeleka mwili kwenye gari kwa safari ya Chasimba kwa mazishi.

ALIYEKUWA Mkuu wa Polisi mkoani Singida (RPC) Peter Charles Kakamba, ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi Jumanne katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, mwili wake uliagwa jana baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika Kanisa Katoliki Parokia ya Muhimbili na kusafirishwa kuelekea kijiji cha Chasimba wilayani Mpanda, Mkoa wa Katavi kwa mazishi.

Marehemu alikuwa akisumbuliwa na tatizo ya utumbo kujikunja ambapo alifanyiwa upasuaji mara kadhaa lakini liliendelea kujirudia mpaka umauti ulipomkuta.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL

halotel-strip-1-1

Comments are closed.