Mambosasa: Kigogo Wizara ya Fedha Amejinyonga, Ameacha Wosia -VIDEO
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema leo Julai 31, 201, kuwa kigogo aliyekuwa mtumishi Wizara ya Fedha, aliyefahamika kwa jina Leopold Kwemba Lwajabe, amejinyonga kutokana na ushahidi uliopo, ikiwemo ‘note book’ aliyoiacha ikielezea mgao wa mali zake zote.
Mambosasa ameyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa familia yake, Lwajabe aliyekuwa mkurugenzi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini kupitia wizara hiyo, mwili wake ulikutwa wilayani Mkuranga mkoani Pwani Julai 26, 2019 ukining’inia katika mti wa mwembe.


Comments are closed.