The House of Favourite Newspapers

RPC MBEYA: UWOYA TUMEMTIA MBARONI

Irene Pancras Uwoya

BAADA ya kusambaa kwa taarifa ya kukamatwa kwa staa wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya na wenzake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (RPC), Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Ulrich Matei amefunguka: “Ni kweli tumemtia mbaroni Uwoya na wenzake.”

 

MBALI NA UWOYA

Uwoya na wasanii wenzake, Tausi Mgedela, Idris Makupa ‘Kupa’, Hamis Changale ‘Mtanga’ na wengineo walikamatwa usiku wa Jumamosi iliyopita ya Septemba 22 kuamkia Septembea 23, mwaka huu baada ya kukutwa wakinywa pombe baa jijini Mbeya wakiwa wamevuka muda wa baa kufungwa. Kwa kawaida sheria zinaonesha kuwa baa inatakiwa kufunguliwa saa 10:00 jioni na kufungwa saa 5:00 usiku, lakini wao hawakujali. Tukio hilo lilijiri usiku mnene kwenye Baa ya Chauls iliyopo maeneo ya Chuo cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya.

 

BAADA YA TAMASHA  WAPOOZA KOO

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, mastaa hao walikwenda jijini Mbeya kwenye Tamasha la Mimi Nimefurahi ambapo baada ya shughuli hiyo ndipo wakazama kwenye baa hiyo kupooza koo na mashabiki wao.

 

Ilidaiwa kuwa, hata hivyo, walipitiliza muda wa kupiga ulabu ndipo walipovamiwa na Polisi waliokuwa doria ambapo waliwatia pingu watu wote waliokutwa wakinywa pombe bila kujali huyu ni staa na huyu siyo staa. “Ilikuwa ni mshikemshike, si unajua tena mastaa wanavyokuwa na ubishi halafu wakishapiga pombe? Ni balaa tupu! “Baada ya mvutano wa hapa na pale ndipo wakarundikwa kwenye difenda la Polisi na kwenda kutupwa selo katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Mbeya,” alisema shuhuda wetu huyo ambaye ni mmoja wa watu waliokuwa kwenye msafara wa ziara hiyo.

Image result for Ulrich Matei

WALALA LUPANGO

Ilielezwa kuwa, Uwoya na mastaa hao wenzake walilala lupango hadi kesho yake ambapo walitolewa jioni kwa dhamana na mtu aliyetajwa kwa jina moja la Fadhil ambaye ndiye aliyewaalika kwenye tamasha walilohudhuria jijini Mbeya.

 

DOGO JANJA VIPI?

Ilidaiwa kuwa ili kujua kama kweli ni mkewe akamsaidie, watu walimtafuta msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kujua atachukua hatua gani, lakini ilisemekana alimpotezea Uwoya. Gazeti hili lilimtafuta Dogo Janja ili kueleza ni kwa nini alimpotezea Uwoya, lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa chating za WhatsApp hakujibu.

 

HUYU HAPA  KAMANDA WA MBEYA

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juu ya tukio hilo juzi Jumatatu, Kamanda Matei alikiri na kusimulia mastaa hao walivyokamatwa na hatma yao, Kamanda Matei alifunguka; Ni kweli tumemtia mbaroni Uwoya, Tausi na hao wenzao.

 

“Walikamatwa na Polisi wa doria baada ya kukutwa baa wakiendelea na mambo yao wakati muda wa kufunga baa umepita. “Tuliwakamata na tulitaka wao ndiyo wawe mfano bora kwa jamii kwa sababu ni kioo cha jamii. “Lakini sikutaka kulikuza jambo hilo kwa sababu lilitokea wakati taifa lipo kwenye msiba mzito uliotokana na ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kule Ukerewe.

 

“Hivyo niliona jambo hilo lisituondoe kwenye maombolezo, kwa hiyo tuliwapa elimu na kuwaachia, lakini liwe ni funzo kwa wengine. “Ni marufuku kunywa pombe muda wa kazi na ni marufuku kupitiliza muda wa kufunga baa.”

Mambo 20 Usiyoyajua Kuhusu Rihanna

Comments are closed.