The House of Favourite Newspapers

Rubani Afariki kwa Mshituko wa Moyo Baada ya Kutua Tabora

0
Stephen Lohay

RUBANI “Stephen Lohay” ambaye ni nahodha nyuma wa shirika la ndege la Air Excel amefariki dunia kwa mshtuko wa moyo baada ya kutua ndege mkoani Tabora.

 

Alipata mshtuko wa moyo akiwa angani lakini kwa ujasiri alifanikiwa kutua ndege hiyo mkoani Tabora kabla ya kufariki dunia.

 

Lohay pia alikuwa Mwenyekiti wa Arusha Motor Sports Club na hadi mauti yalimkuta alikuwa akijiandaa na mashindano ya Kitaifa ya Mbio za Magari katika Mkoa huo.

Juhudi za kumsafirisha hadi Dar es Salaam ziligonga mwamba

Ripoti za awali kutoka AMSC zilieleza kuwa alikuwa Rubani Mkuu katika kampuni ya uchukuzi ya Air Excel.

 

Juhudi za kumsafirisha Rubani huyo hadi Dar-es-salaam hazikufua dafu kwani alifariki muda mfupi baada ya kutua.

Leave A Reply