The House of Favourite Newspapers

RUBY ACHIA DUDE JIPYA, ‘NIWAZE’

Ruby akiimba. 

MWANADADA kutoka kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ baada ya kukaa kimya kwa muda amekuja na video yake mpya iitwayo ‘Niwaze’.

Ruby akipozi.

Ngoma hiyo ameizindua usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Club Next Door jijini Dar es Salaam, ambapo ndani ya wimbo huo ameshirikiana na vijana watatu wa  kundi la The Mafik.

Mmoja wa The Mafik akiimba.

Ruby ameelezea kuwa kolabo hiyo aliyofanya ni baada ya kuwaona vijana hao wapo vizuri katika muziki na akasema video hiyo hakika mashabiki wake wata-enjoy kuitazama kwani maudhui yake yanaendana kabisa na kilichoimbwa.

Ruby akiwa na baadhi ya vijana alioimba nao wa The Mafik.

Video hiyo imeitengenezea nchini Afrika Kusini na tayari inapatikana katika mitandao ya kijamii kuanzia jana ilipozinduliwa.

NA DENIS MTIMA | GPL

Comments are closed.