MWANADADA anayefanya poa kwenye gemu ya Muziki wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ amefungukia madai ya kutimuliwa na uongozi wake, Tanzania House of Talent ‘THT’ kuwa mengi yanasemwa lakini ukweli ni kwamba hajatimuliwa.
Akipiga stori na Over Ze Weekend Ruby anayetamba sasa na Wimbo wa Forever alisema kuwa;
“Mambo yangu yanaenda vizur, THT nimetoka nayo mbali sioni sababu ya kuongelea ishu hiyo ili watu wazidi kuzusha wanayoyajua ni bora nikae kimya maana hayo ni mambo yangu binafsi,” alisema Ruby.


