The House of Favourite Newspapers

Saa9 Usiku…Bata la MOBETO, mama’ke acha kabisa

DAR ES SALAAM: Fedha inaongea! Wakati watu wengine wakilia ukata, mwanamitindo wa Bongo, Hamisa Mobeto na mama’ke, Shufaa Rutiginga wamenaswa majira ya saa 9:00 usiku wakila bata la hatari hadi kuku wakaona wivu.

Wawili hao walinaswa hivi karibuni katika Tamasha la Masauti Luxury lililofanyika Life Club Mwenge jijini Dar ambapo bata lao lilikuwa ni balaa.

 

Katika tukio hilo, Mobeto na mama’ke wakiwa na kundi la wapambe wao, waliingia ukumbini hapo na kukaa sehemu ya watu maarufu ‘V.I.P’ ambapo meza yao ilipambwa na mazagazaga kibao vikiwemo vinywaji na minofu.

Katika kuonesha mama na mwanaye huyo kwa sasa wako njema mfukoni, walikaa kwenye masofa na kundi la wapambe zaidi ya sita ambapo gharama zote zilikuwa zikitoka kwenye pochi nene ya Mama Mobeto.

 

Mama huyo kwa kuonesha jeuri na kwamba kwa sasa fedha haimpigi chenga, mwanamuziki Christian Bella alipopanda jukwaani na kuanza kuimba hasa kilipopigwa Kibao cha Nani Kama Mama, mara kadhaa alikuwa akiwapa pesa wapambe wakamtunzie huku mwenyewe akimpa ‘hai’ Bella kwa kumpungia mkono kwa mbali.

Kama inavyokuwa kwa mapedeshee, Bella alikuwa akitumia muda mwingi kuwapaisha majina yao na alipoona haitoshi aliliacha jukwaani na kwenda walipokaa na kuwaimbia na kucheza nao.

 

Wote kwa pamoja walianza kuserebuka sehemu hiyo huku wakiwa wameshikana ambapo Mama Mobeto alitoa pochi nene na kumtunza Bella noti nyekundu, hali iliyozua shangwe ukumbini hapo.

Hali hiyo ilisababisha umati uliofurika kuanza kuwajadili Mobeto na mama’ke kwa jinsi maisha yao yalivyobadilika ghafla na kugeuka mapedeshee

Stori: RICHARD BUKOS, IJUMAA

Comments are closed.