The House of Favourite Newspapers

Safari za Treni Zasitishwa Ukanda wa Kaskazini

SHIRIKA la Reli Nchini limewataarifu wateja wake na kuwaomba radhi kutokana na kusitishwa kwa huduma za usafirishaji mizigo katika ukanda wa Kaskazini yaani mikoa ya Kilimanjaro na Tanga kuanzia Oktoba 26, 2019.

Limeeleza kuwa usitishwaji huo ni kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika ukanda huo na kusababisha mito ya Pangani (Ruvu na Rwengera) kujaa maji na maji hayo kuelekea relini.

Maji hayo yamesababisha uharibifu wa miundombinu yakiwemo madaraja ambapo sehemu zilizoathirika ni Muheza, Korogwe hadi Mombo kipande kilichoharibika madaraja mawili na Wami – Makinyumbi (Hale) kipande kilichoharibika makaravati manne.

Aidha, Shirika limesema linaendelea na jitihada za ukarabati na litatoa taarifa njia itakapotengamaa na kurejea kwa usafiri kama awali.

Comments are closed.