The House of Favourite Newspapers

Saida Kaloli: Nilitumika Kuwanufaisha Wengine

MWANAMUZIKI Saida Kalori amefunguka baada ya kimya kingi kwenye muziki ambapo amesema enzi zake wakati anaimba alikuwa akitumika na watu wengine.

Watu hao walinufaika zaidi kuliko yeye, kwani licha ya kufanya vizuri kimuziki miaka kadhaa iliyopita, hakupata chochote na bado anaishi katika mazingira magumu.saida-kalori

Saida Kalori.

“Niliumizwa kuanzia mwanzo, ni vitu vichache nilivyovipata, kama mkibahatika waandishi wa habari wenye makamera na wakija kwangu watashuti kulingana na nilivyo, wataona mazingira ninayoishi ndipo watanzania watazidi kufunguka zaidi.”

Kwa sasa Saida Karoli anaishi jijini Mwanza. Hivi karibuni amerejea tena kwenye midomo ya watu baada ya mwanamuziki Diamond kurudia wimbo wake Salome uliowahi kutesa mwanzoni wa miaka ya 2000.

CREDIT: JEMBE FM.

 

Comments are closed.