The House of Favourite Newspapers

Sakata la Ushoga: Benki ya Dunia Kusitisha Ziara Zake Tanzania

BENKI ya Dunia  imeungana na nchi kadhaa duniani zinazoishutumu Tanzania kuhusiana na kile kilichotajwa kuwa ni kuwadhalilisha mashoga ambapo imeamua kusimamisha ziara zake hapa nchini.

 

“Kutokana na matukio nchini Tanzania ambako mashoga na watu wengine wanaofanya mapenzi ya jinsia moja wanadhalilishwa na kubaguliwa, ziara zote za kwenda Tanzania zimesimamishwa mara moja  hadi tutakapohakikishiwa usalama wa wafanyakazi wote,” imesema sehemu ya hati iliyotolewa na benki hiyo.

 

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1947, Benki ya Dunia imetoa fedha kwa miradi ya maendeleo zaidi ya 12,000 nchini Tanzania kupitia mikopo na misaada ya aina mbalimbali.

 

Sakata la mashoga nchini lilipamba moto wiki kadhaa zilizopita baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuamua kuchukua hatua dhidi ya watu wenye tabia ya ushoga, jambo ambalo limeibua hisia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukoselewa na jumuia ya kimataifa.

 

Serikali ya Tanzania imesema hatua za kiongozi huyo wa mkoa ni maoni yake binafsi, na kwamba serikali itaendelea kuheshimu haki za binadamu wote kama iliyo katika katiba ya nchi yake.

LUGOLA: VIUNGO vya SHOGA ni vya Haja/ Wanakiuka Matumizi Yake

Comments are closed.