The House of Favourite Newspapers

Samatta Aondoka na TECNO CX Mpya ya Global Insta

Mwaitanga Samatta (kushoto), akikabishiwa zawadi ya Tecno Camon CX na Meneja TEHAMA wa Global Publishers, Edwin Lindege.

KAMPUNI YA Global Publishers kupitia shindano lake la Global Insta imemkabidhi zawadi Baraka Michael (brity59) ambaye ni mshindi wa Simu mpya ya kisasa smartphone aina ya Tecnoi Camon CX ambaye ameshinda baada ya kuwabwaga wenzake 53.

 

Baraka mkazi wa Tabora ambaye katika akaunti yake ya Instagram anatumia jina la brity59 aliwakilishwa na mjomba wake, Mwaitanga Samatta mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam ambaye alifika katika Studio za Global TV Online kumwakilisha yake huyo na kumchukulia zawadi yake baada ya mhusika kushindwa kufika Dar.

 

Akizungumza mara baada yakukabidhiwa zawadi hiyo, Samatta alikuwa na haya ya kusema;

“Nawashukuru sana Global Publishers kwa nzawadi hii, nimeamini kweli katika mashindano yao wanatoa zawadi bila upendeleo tena kwa uwazi. Mimi hata ndugu yangu Baraka (mshindi) hakuna mtu tunayemfahamu hapa Global Publishers, lakini wamechezesha droo bila upendeleo na mshindi akapatikana. Hivyo niwasihi Watanzania washiriki katika mashindano haya na wazidi kufuatilia mitandao ya kijamii ya Global Publishers kwa habari na matukio mbalimbali.”

Mwaitanga Samatta baada ya kukabidhiwa zawadi.

Kwa upande wake, Meneja wa Tehama wa Global Publishers, Edwin Lindege alisema;

“Nawashukuru mashabiki wetu kwa kuendelea kuwa nasi, tunawaahidi hatutawaangusha, tutaendelea kuwapasha habari kwa kuzingatia weredi wa taaluma hii. Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha tunapata habari bora zaidi na kwa wakati, matukio ya papo kwa hapo, habari za burudani, michezo na nyingine zote.

“Endeleeni kuwa karibu na mitandao yetu ya Instagram @GlobalPublishers, Facebook @GlobalPublishers, Twitter @GlobalHabari, YouTube chaneli ya Global TV Online, website ya www.globalpublishers.co.tz na Application yetu mpya ya Global Publishers yenye kila kitu unachokijua kuhusu tasnia ya habari. Hii inapatikana kupitia App Store na Play Store.

 

Katika droo hiyo iliyochezeshwa kwa wazi, droo tano ndogo zilichezeshwa ambapo washindi wa kila droo waliingizwa kwenye droo kubwa ya fainali ambayo mshindi mmoja aliyejulikana kwa jina la brity59 ndiye amejinyakulia simu hiyo.

 

Samatta Aondoka na TECNO CX Mpya ya Global Insta

Comments are closed.