The House of Favourite Newspapers

Sanchi Aanza na Mabadiliko ya Mavazi

MWANAMITINDO mwenye umbo tata, Jane Rimoy ‘Sanchi’ amefunguka kuwa mwaka huu ameuanza kwa mabadiliko ya mavazi ambapo anavaa nguo ndefu mpaka miguuni ambazo nazo zinamfanya kuwa mrembo.

 

Akibonga na Wikienda, Sanchi alisema amejichunguza na kujiona kuwa anapovaa nguo ndefu anaonekana nadhifu zaidi na mwenye mvuto wa kipekee hivyo ameamua kubadilika mwaka huu na kuvaa nguo hizo na anaamini kila mtu atamzoea hivyo.

 

“Unajua kila kitu mtu hujaribu kukifanya, lakini kwa upande wa nguo nimegundua kuwa ndefu pia zinanipendeza zaidi hata nikiende kwenye hafla mbalimbali navaa naonekana msichana wa nguvu tena mwenye heshima zake,” alisema Sanchi.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.