The House of Favourite Newspapers

Sasa Anajiita Abu Hayyan, A.K.A Ostaz Juma

ostadh-juma-namusoma-1

MFADHILI wa kitambo katika masuala ya muziki wa kizazi kipya ameamua kubadili jina na kuwaomba wadau wake wamtambue kwa jina la Abu Hayyan, a.k.a Ostaz Juma Namusoma.

ostadh-juma-namusoma-2Abu Hayyan, a.k.a Ostaz Juma Namusoma.

Aidha, Abu amesema kuwa hata kwa upande wa mavazi ameamua kubadilika na kupendelea kuvaa vazi la kanzu zaidi kuliko mavazi mengine.

“Napenda kuwafahamisha wadau kuwa kwa sasa napenda nitumie jina la Abu Hayyan, jina ambalo nimeliona ni la kipekee linalo nasibiana (linalofanana) na mtoto wangu, Hayyan Juma, kwa hiyo napenda niitwe hivyo a.k.a Ostaz Juma Namusoma,” alisema Ostaz.

ostadh-juma-namusoma-3

Kifafanua maana ya jina hilo, alisema kuwa asili ya jina hilo ni arabuni. Abu maana yake ni Baba na Hayyan ni jina la mtoto wake wa kwanza wa kiume, hivyo ni sawa na kumuita Baba Hayyan.

Abu amesema kuwa kwa sasa yuko nchini Oman katika jiji la Muscat akipumzika na kubadilisha hali ya hewa, amedai nchi hiyo ni miongoni mwa nchi anazozipenda sana.

“Nipo Mji wa Muscat nchi ya Oman na hapo (pichani) nipo katika Qasri ya Qabus, Mfalme wa Oman na huku nimekuja kutembea kidogo na kubadilisha hali ya hewa kwani ni nchi niliyo ipenda kiukweli, kwani haina  zogo kama ilivo Dubai na Qatar”, alisema Abu Hayyan a.k.a Ostaz Juma.

halotel-strip-1

Comments are closed.