The House of Favourite Newspapers

Serengeti Boys Yazitibulia Yanga na Simba

Kikosi cha timu ya Yanga.

 

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limepangua ratiba ya mechi za leo Jumatano za Ligi Kuu Bara ambapo Simba itacheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga na Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar.

 

Mechi hizo awali zilipangwa kuchezwa kuanzia saa 10:00 jioni, lakini sasa zitaanza saa 8:00 kutokana na kupisha mechi ya Serengeti Boys dhidi ya Uganda ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17.

 

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Boniface Wambura, ameliambia Championi Jumatano kuwa, mechi hizo zote kwa pamoja zitachezwa leo saa 8:00 mchana badala ya saa 10:00 kama ilivyokuwa hapo awali.

 

Wambura alisema wamefi kia uamuzi huo ili kupisha mchezo huo wa Serengeti Boys na Uganda ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kuanzia saa 11:00 jioni.

“Kwa hiyo kutokana na hali hiyo, mechi zote hizo zitaanza saa 8:00 mchana badala ya saa 10:00 kama ilivyokuwa hapo awali. “Tayari timu zote tumeshazipatia taarifa kuhusiana na mechi hizo, ni matumaini yetu kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa,” alisema Wambura.

 

Kwa upande wa Yanga, mratibu wa timu hiyo, Hafi dh Saleh, amethibitisha kuhusiana na mabadiliko hayo huku akisema kikosi chao kipo tayari kwa kucheza mechi hiyo katika muda huo katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Wakati Yanga wakicheza Morogoro, Simba wao watacheza kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga dhidi ya wenyeji wao, Coastal Union.

Comments are closed.