The House of Favourite Newspapers

Serikali kutoa kadi za kuingilia uwanjani bure

nape-2

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) akiongea jambo katika semina elekezi ya matumizi ya kadi za kielektroniki iliyofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Michezo Tanzania, Nkenyenge Felix na Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando.

nape-3

Nape Nnauye akiendelea kufafanua jambo.

nape-4

Meneja wa Mipango wa Selcom, Gallus Runyeta akafafanu jambo katika semina hiyo.

nape-5

Baadhi ya waandishi wa habari waliouhudhulia semina hiyo. 

Sweetbert Lukonge

BAADA ya hivi karibuni serikali kufunga mashine za kielektroniki katika Uwanja wa Taifa, kadi kwa ajili ya kuingilia uwanjani humo kutolewa bure.

Serikali iliamua kufunga mashine hizo katika uwanja huo ili kuondokana na mfumo wa zamani wa kutumia tiketi za kawaida kwa lengo la kulinda mapato yake uwanjani hapo ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa yakiishia mifukoni wa wajanja wacheche.

Akizungumza na katika semina elekezi ya jinsi ya kutumia mfumo huo  mpya wa kuingia uwanjani humo uliyozinduliwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, NapeNnauye, Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom ambayo ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamia mfumo huo, GallusRunyeta alisema kuwa kadi zitakazokuwa zikitumika katika mfumo huo zitatolewa bure.

Alisema kadi hizo zitaanza kutolewa hivi karibuni ambapo kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika katika uwanja huo ambao serikali kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania watauandaa kabla ya mchezo wa Simba na Yanga.

“Watu ambao watapata kadi hizo ni wale ambao watanunua tiketi kwa ajili ya mechi hiyo baada ya hapo tutaanza kuziuza.

“Hata hivyo mbali na kadi hizo kuzitumia uwanjani pia aliyenayo anaweza kuitumia kwa matumizi mengine kama vile kuhifadhi fedha lakini pia inamwezesha mtu huyo kulipia bidhaa na huduma mbalimbali kama kufanya malipo ya mtandaoni pamoja na kulipa bili kwa wakala wa Selcom au sehe yoyote biashara yenye mashine ya POS ya Selcom, “ alisema Runyeta.

Wakati huohuo, Nnauye ameuagiza Naibu Mkurugenzi wa Mchezo Tanzania, Nkenyenge Alex kuhakikisha anaandaa sera ya michezo nchini mapema iwezekanavyo mpaka kufikia mwezi Septemba iwe tayari.

Alisema lengo kubwa la kufanya hivyo ni kutaka kuleta mapinduzi makubwa ya michezo hapa nchini kwani sera ilie iliyopo hivi sasa imeshapitwa na wakati.

“Nataka mpaka kufukia mwezi Septemba sera hiyo iwe tayari kama utashindwa kufanya hivyo basi ukatafute sehemu nyingine ya kufanya kazi pamoja na wenzako wote,” alisema Nnauye.

Comments are closed.