The House of Favourite Newspapers

SHAKIRA YAMKUTA

MWANAMUZIKI anaye-tikisa kwa kukata nyonga, Shakira yamemkuta baada ya kudaiwa kukwepa kodi kiasi cha dola za Kimarekani 16.5 (zaidi ya shilingi bilioni 38 za Kibongo).

 

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne iliyopita na Mahakama ya Catalonia, mwanamuziki huyo mwenye asili ya Colombia alitakiwa kulipa kodi kipindi cha mwaka 2012 na 2014 lakini alikwepa.

 

Mwakilishi wa Shakira, alimtetea mwanamuziki huyo kuwa katika kipindi hicho hakuwepo Hispania hadi mwaka 2015 kwa hiyo hizo taarifa hazina ukweli.

 

Mastaa wengine waliokumbwa na msala wa kukwepa kodi ni wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Hispania, Gerard Pique na Lionel Messi ambapo walilipa faini ya shilingi milioni 668.

CATALONIA, HISPANIA

Comments are closed.