The House of Favourite Newspapers

SHIGONGO AHUDHURIA NDOA YA MPWA WAKE MWANZA

MC wa hafla hiyo akimtambulisha Shigongo kwa wageni waalikwa.
Emmanuel na Christina wakijiandaa kukata keki.
Shigongo ( wa pili kushoto) akifuatilia kilichokuwa kikiendele.
Shigongo akipokea keki kutoka kwa mpwa wake.
Shigongo akisalimiana na dada yake kwa kumpa pongezi za mwanaye kufikia hatua hiyo ambaye ni mama wa bwana harusi.
…Akizungumza jambo mbele ya  wageni waalikwa.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.

 

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Global Group, Eric Shigongo amehudhuria hafla ya sherehe ya mpwa wake aitwaye, Emmanuel Aron.

 

Hafla ya sherehe hiyo inafanyika usiku huu baada ya mchana kufungwa kanisa la Katoliki la Nundu- Meco na  inafanyika ndani ya ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest ya Jijini Mwanza.

 

Shigongo akimuasa mpwa wake amesema kuwa familia yao  ipo imara katika kuhakikisha  familia ya Emmanuely na Christina inakuwa katika misingi ya dini na ya kumpendeza mwenyezi mungu.

 

Alisema kuwa hategemei kuona mpwa wake Emmanuel akimbadilikia  mkewe  na ahakikishe wanavumiliana kwa shida na tabu kama maandiko yasemavyo, yeye hatasita kuwasaidia pale patakapohitajika msaada.

Comments are closed.