Shigongo Alia na Uzembe wa Serikali Kutofuatili Matumizi ya Pesa za Umma

Mbunge wa Jimbo la Buchosa Erick Shigongo

MBUNGE wa Jimbo la Buchosa kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Erick Shigongo ameishauri Serikali kuweka mfumo thabiti wa kufuatilia matumizi ya pesa za Serikali kwenye miradi ya Umma kutokana na kuwepo kwa matukio kadhaa ambayo yanaonesha pesa nyingi za Serikali zikipotea kutokana na kutofuatiliwa matumizi yake.

 

Shigongo ameyasema hayo akichangia hoja kwenye Bunge la 12 la Bajeti Kuu linaloendelea Jijini Dodoma, huku akimshauri Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kuhakikisha Serikali inachukua hatua kudhibiti upotevu huo wa mali za umma.

 

Kwa upande mwingine Shigongo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kuidhinisha kiasi cha bilioni 20 kwa ajili ya zoezi la Anwani za makazi zoezi ambapo kwa mujibu wa Shigongo limekamilika kwa asilimia 95.

Shigongo amecharuka Bungeni

Lakini pia Shigongo ameishauri Serikali iweze kuimarisha taasisi nchini ili ziweze kufanya kazi zake kwa ufanisi ikiwemo Taaisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ambayo kwa nafasi kubwa inaweza kusaidia kudhibiti upotevu mkubwa wa mali za Umma ikiwemo pesa zinazotumika kwenye miradi mbalimbali ambazo nyingi zinaingia kwenye mifuko ya watu badala ya kukamilisha miradi.2176
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment