The House of Favourite Newspapers

Shigongo, TARURA Wambana Mkandarasi Buchosa – Video

0

MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, ameambatana na Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Mwanza baada ya kufanya ziara ya kukagua barabara zinazotengenezwa na TARURA ambapo wamekuta hali siyo nzuri kwa wakandarasi husika kutengeneza barabara chini ya kiwango, jambo ambalo limewakera.

 

 

 

Katika ziara hiyo wametembelea barabara ya Nyakaliro kwenda Kanyara ambayo eneo kubwa la barabara hiyo bado halijatengenezwa huku muda wa mkandarasi ukielekea kuisha tarehe, yaani Machi 20, mwaka huu.

 

 

 

Ziara hiyo iliendelea katika barabara ya Lupalanyonga ambayo nayo bado haijakamilika, pia walitembelea barabara ya Kalebezo kwenda Katoma ambapo walikuta daraja likiwa limevunjika kwenye barabara hiyo huku ikiwa haijaanza kufanyiwa matengenezo yoyote.

 

 

 

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Mratibu wa TARURA Mkoa wa Mwanza amemsisitiza mkandarasi huyo kumaliza kazi hizo kwa wakati uliopangwa huku akisisitiza kutoongeza muda kwani wametumia muda mwingi bila kukamilisha ujenzi wa barabara hizo.

 

 

 

Shigongo amewataka TARURA kuwa wakali kwa wakandarasi ambao wanachezea fedha za serikali kwani Rais Magufuli anazitafuta kwa kuhangaika sana lakini watu wa chini wanafanya uzembe.

 

 

 

“Kwa hili mimi kama mbunge niliyechaguliwa na wananchi sitokubali fedha za serikali zichezewe kwenye jimbo langu. Ninachowaomba TARURA ni kwamba fedha kidogo mnazopata zitumieni vizuri kukamilisha barabara zetu.

 

 

 

“Sisi kama wabunge tunapambana kuona bajeti yenu inaongezeka ili muweze kutekeleza miradi vizuri, naomba hilo lizingatiwe,” amesema.

 

 

 

 

 

 


Leave A Reply