The House of Favourite Newspapers

Shigongo: Wasio na Form Four Waruhusiwe Kusoma Vyuo – Video

0

MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo ametoa mapendekezo yake kuhusu muswada wa maboresho ya mfumo wa elimu nchini akiitaka wizara husika kupitia baadhi ya vipengere na kuwaruhusu watu wenye vipaji na waliofanya mambo makubwa katika Taifa hili  kutambuliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) pamoja na Baraza la taifa la Elimu na Ufundi (NACTE).

 

“Wapo watu kwenye Taifa hili, kwa uzoefu wao wamefanya mambo makubwa sana, hata hapa Bungeni wapo watu hawana elimu lakini wamefanya mambo makubwa. Tungeomba watu hawa watambuliwe na mfumo wetu wa elimu ili waweze kujiendeleza na kupata maarifa zaidi kulisaidia Taifa letu.

 

“Nchi yetu isifunge milango kwa watu ambao hawakupata formal education ili wapate masomo ya elimu ya juu. Ningependekeza mtu aliyetambuliwa na TCU au NACTE akasome popote bila kuulizwa cheti cha form four.” – Mhe. Eric Shigongo.

Leave A Reply