The House of Favourite Newspapers

Shika Ndinga ya EFM Yaja kivingine 2018

Meneja Mkuu wa Efm, Dennis Busulwa akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Simu  (TTC), Nicodemus Mushi, ambao ni wadhamini wa Shindano la ‘Shika Ndinga’ akielezea udhamini wao.
Ofisa Uhusiano wa  Chotec, Patronila Mtatiro, ambao ni wadhamini wa Shindano la ‘Shika Ndinga’ naye akielezea udhamini wao
Mmoja wa washindi wa Shindano la Shika Ndinga wa mwaka jana akielezea mafanikio yake aliyoyapata tokea kuwa mshindi wa gari 2017.
Mshindi mwingine wa 2017 wa Shindano la Shika Ndinga akizungumzia  mafanikio yake hadi sasa.

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.

KITUO cha Redio cha Efm kimetimiza miaka minne tangu kilipoanzishwa  mwaka 2014,  kikiwa na wafanyakazi kumi ambapo kwa sasa kinakadiliwa kuwa na wafanyakazi miamoja.

 

Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Efm, Dennis Busulwa ambaye  ameeleza kuwa kituo hicho kimeweza kusikika masafa yake katika mikoa sita ambayo ni, Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, Mwanza,Tanga na Mtwara.

 

“Efm redio tunapenda kuishukuru serikali na wadau wake akiwemo msikilizaji wetu kwa kuendelea kutuunga mkono katika kipindi chote hicho ambapo tunasherehekea miaka mine, tumeongeza masafa yetu kutoka mikoa sita hadi mikoa kumi ambayo ni Dodoma, Morogoro, Tabora, na Kigoma,” amesema.

 

Aidha kituo hicho cha redio kimezindua msimu mwingine  mpya wa shindano la ‘Shika Ndinga 2018’ baada ya kufanyika mwaka jana na kupatikana washindi.

 

“Shindano hili sasa ni kwa mwaka wa nne, na lengo ni kumwezesha msikilizaji kunufaika na zawadi tunazozitoa ikiwemo gari na pikipiki, pia kushirikisha jamii ambayo ndiyo walaji wakuu wa bidhaa zetu pamoja na kutoa shukrani kutokana na mchango wake katika ukuaji na usikilizwaji wa redio yetu,” alisema.

 

Aliongeza kuwa, sababu nyingene ya kusherehekea miaka minne  ya Efm ni kuzaliwa kwa kituo cha televisheni cha TVE, na kwamba wasingelifika hapo walipo kama  isingelikuwa msaada kutoka taasisi na sekta mbalimbali ikiwemo serikali kwa kuwapatia vibali vya kufungua redio.

 

Comments are closed.