The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba… Muda Unakimbia, Nyumba Inakusubiri

0

NYUMBA (17) Na Mwandishi Wetu

SIKU zote, muda huwa ni mali, ndiyo maana kwa wenye weledi zaidi, huona ni afadhali wapoteze fedha kuliko wakati, maana hela unaweza kupata zingine, lakini muda ukishaenda, haurudi.

Ndiyo maana wahenga wakatuambia kuwa lenye kuwezekana leo, lisingoje kesho kwa sababu nani ajuaye, kwanza kama kesho yenyewe utafika au hilo jambo lenyewe litakuwa katika nafasi na ubora uleule wa leo?

Sasa basi, muda wa kufika tarehe ya droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba unakaribia, maana ni mwisho wa mwezi huu ndiyo inafanyika. Mshindi wake hajulikani kwa sababu kuponi zipo nyingi, maelfu kwa maelfu, lakini siku zote mwenye siri juu ya ipi itanyakuliwa na kutangazwa mshindi ni Mungu pekee.

1.Msomaji wa Gazeti la Amani, Crispin Rojas (kushoto) akijaza kuponi yake ili kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba. Katikati ni Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda.Zinaweza kuwa hizo ambazo tayari unazo, au zinaweza kuwa hizi unazoziacha hivi sasa kwa kutonunua gazeti zinazotolewa na Global Publishers ambazo ni Championi, Uwazi, Ijumaa, Risasi, Ijumaa Wikienda na Amani.

Nani ajuaye, huenda kuponi ya ushindi bado haijanunuliwa na pengine wewe ndiye unayesubiriwa umiliki nyumba hiyo iliyopo Salasala jijini Dar es Salaam ikiwa na thamani ya shilingi milioni 60, ndani ikiwa na samani zake zote muhimu.

Ni mjengo wa kisasa uliojengwa eneo tulivu na muonekano wake, unakupa raha ya kuwa mmiliki wake. Pamoja na thamani kubwa, lakini wewe unaweza kuupata kwa kununua gazeti lako kwa shilingi mia tano tu, kasoro lile la Ijumaa ambalo limeboreshwa na sasa linauzwa kwa shilingi elfu moja tu.

Nyumba (9)Kama nilivyodokeza pale awali, muda unakimbia kwa kasi ya ajabu wakati nyumba ipo tu inakusubiri, fanya uamuzi wa busara kwa kujaribu bahati yako, maana unaweza kujilaumu kwa kumuona jirani yako akiipata nyumba hii, kwa vile alikuwa ananunua kuponi kila mara na wewe ukawa ukimcheka kwa kutoamini kama kweli Global Publishers wanaweza kufanya kitu kama hiki.

Tumesisitiza mara kwa mara na leo tunarudia tena, nyumba hii itatolewa kwa mshindi atakayetokana na kuponi itakayochukuliwa ndani ya pipa lililozungushwa, mbele ya ushuhuda wa maofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha kwa mujibu wa sheria.

Kama ulikuwa bado hujaanza kununua kuponi, hujachelewa, muda huu wa wiki mbili unaweza kuwa wa miujiza kuliko miujiza yote uliyowahi kufikiri, jaribu leo!

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply