The House of Favourite Newspapers

Simba: Tunapambana na Vita siyo Al Ahly tu

Wachezaji wa timu ya AS Vita.

OFISA Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Simba, Crescentius Magori, ametamba kuwa matokeo mabaya waliyoyapata wapinzani wao AS Vita na JS Saoura yamewapa matumaini ya wao kufuzu katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Kauli hiyo aliitoa juzi baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam walipotokea Misri kucheza na Al Ahly katika mchezo wa hatua ya makundi ya michuano hiyo na Simba kufungwa mabao 5-0.

Timu ya Simba.

Mchezo wa AS Vita na JS Saoura ulimalizika kwa matokeo ya sare ya kufungana mabao 2-2 ambayo Simba kama ikifanikiwa kupata ushindi kwenye michezo yake miwili ya nyumbani itakuwa na matumaini ya kufuzu.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Magori alisema matokeo hayo ya sare kati ya AS Vita na Saoura yamewarudisha mchezoni kutokana na uchache wa pointi walizoachana katika kundi lao D.

 

“Mashabiki wa Simba wasikatishwe tamaa ya kufuzu hatua inayofuata ya michuano hii, kikubwa wanachotakiwa ni kuungana kwa pamoja na kuweka mikakati thabiti ya ushindi ya michezo yote miwili tutakayocheza hapa nyumbani.

 

“Ukiangalia kwenye kundi letu, Al Ahly pekee ndiyo yenye nafasi ya kufuzu hadi hivi sasa ambayo imejikusanyia pointi saba ikifuatiwa na AS Vita yenye nne tukifuatiwa na sisi wenye tatu.

 

“Hivyo, utaona ni jinsi gani bado tuna nafasi ya kufuzu hatua inayofuata, hivyo sisi Simba na AS Vita tunagombania nafasi moja ya kufuzu na yeyote ana nafasi ya kufuzu kwa atayepata matokeo mazuri katika michezo yake ijayo,” alisema Magori.

Comments are closed.