The House of Favourite Newspapers

Simba Wamtambulisha Mrithi wa Mayanja

0
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara (katikati) akiongea na wanahabari kulia ni Kocha mpya  wa Simba aliyetoka timu ya Rayon Sport ya Rwanda, Irambona Masoud Djuma.

BAADA ya kupita siku moja tangu kocha msaidizi wa timu ya Simba, Jackson Mayanja, raia wa Uganda aamue kujiweka pembeni kukinoa kikosi hicho, hatimaye uongozi wa timu hiyo umemalizana na aliyekuwa kocha wa Rayon Sport ya Rwanda, Irambona Masoud Djuma,  kwa ajili ya kubeba mikoba ya Mganda huyo.

Kocha mpya Rayon Sport ya Rwanda, Irambona Masoud Djuma (katikati).

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo, Djuma aliweka hadharani kuwa amekuja katika kikosi hicho kwa ajili ya kufanya kazi na kukisaidia kufanya vizuri kwenye kila kombe watakaloshiriki.

…Akiongea na wanahabari.

“Nimekuja hapa Simba kwa ajili ya kaufanya kazi tu, na nataka tushirikiane ili timu iweze kusonga mbele itoke hapa ilipo, na pia nipo hapa ili kukuza jina langu maana kiukweli unapozungumzia Simba unazungumzia juu ya klabu kubwa hapa nchini,” alisema kocha huyo.

…Wakipiga picha ya pamoja.

Lakini pia uongozi wa Simba chini ya Kaimu Rais wake, Salim Abdallah ‘Try Again’,  umemteua Richard Robert kuwa meneja wa kikosi hicho akichukua mikoba ya Cosmas Kapinga ambaye aliamua kubwaga manyanga hivi karibuni.

Haji Manara akiongea jambo na kocha msadizi mpya wa Simba, Masoud Djuma.

NA MUSA MATEJA/GPL

Spoti Hausi LIVE: Timu Ya Man City Yatabiriwa Ubingwa wa EPL, Yanga na Simba Tanzania

Leave A Reply