The House of Favourite Newspapers
gunners X

SIMBA YAPIGWA, YAONDOLEWA SPORTPESA SUPER CUP

KLABU ya Simba yenye Maskani yake Mtaa wa Kariakoo jijini Dar es Salaam Leo hii imeondoshwa katika mashindano ya Sportpesa Super Cup na Timu ya Bandari ya nchini kenya kwa jumla ya Magoli 2-1, nchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa.

 

Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere ndiye aliyekuwa wa kwanza kufungua kalamu ya magoli katika mchezo huo kwa kuiandikia goli la kwanza timu yake ya Simba mnamo dakika za Nyongeza kipindi cha kwanza na kuifanya Simba sc kwenda mapumziko ikiwa inaongoza.

 

Kipindi cha pili Bandari waliweza kupata bao dakika ya 59 kupitia penalti iliyopigwa na William Waydi hiyo ilitokana na Mzamiru Yassin kufanya madhambi katika eneo la hatari na alitolewa nje ya uwanja baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Jonas Mkude.

 

Bandari waliendelea kulisakama lango la Simba huku wakijilinda zaidi na mnamo dakika ya 75 waliweza kupata goli la 2 na laushindi.

 

Kwa matokeo hayoBandari inakuwa Timu ya Kwanza kukata tiketi ya kuingia Fainali za Sportpesa huku Timu ya Simba SC inasubiri kucheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Mbao/Kariobang Sharks.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.