The House of Favourite Newspapers

Mkongo Ataja Kinachowamaliza Yanga

Mwinyi Zahera.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa wachezaji wake wanaposhambulia wakiporwa tu mpira basi wanakuwa wazito kurudi nyuma kukaba, jambo ambalo linasababisha mabeki wake kuwa wachache ndiyo maana wamekuwa wakifungwa michezo yao ya hivi karibuni.

 

Yanga hivi karibuni imepoteza michezo miwili kutokana na uzembe katika safu ya ulinzi, ikiwemo mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United na ule dhidi ya Kariobangi kwenye michuano ya SportPesa.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, kocha huyo raia wa DR Congo amesema kuwa wacheza­ji wake wa mbele wanaposham­bulia wakinyang’anywa mpira wanakuwa wazito kushindwa kurudi.

Zahera hivi karibuni kikosi chake kimeweza kupoteza mchezo wao huku uzembe ukionekana katika safu ya ulinzi.

“Nilichogundua katika michezo ya hivi karibuni kwa nini tumeshindwa ni kutokana na kitendo cha wachezaji pale wana­pokimbilia kushambulia wakiporwa tu mpira na wapinzani basi wanakuwa wazito kurudi, jambo ambalo linawafanya mabeki kuwa peke yao na kuelemewa na kupeleka wapinzani kutumia hiyo nafasi.

 

“Sasa hapo unakuta mzigo mkubwa unakuwa kwa mabeki ambao wana­kuwa peke yao ndiyo maana wanazidiwa na wapinzani jambo amba­lo linatakiwa kufanyiwa kazi kwa kiasi kikubwa,” alisema Zahera.

 

Ikumbukwe Yanga inatarajiwa kucheza na Biashara United, Januari 31, mwaka ukiwa ni mchezo wa Kombe la FA.

Comments are closed.