The House of Favourite Newspapers
gunners X

Singeli Michano Yatikisa Bagamoyo

efm-1

Baadhi ya washiriiki wa Muziki wa Singeli Michano wakionyeshana uwezo jukwaani.

efm-2 efm-3

Wakazi wa Bagamoyo na wasikilizaji wa Efm Redio wakiwa kwenye Jogging.

Tamasha la Muziki Mnene, juzi Novemba 5, mwaka huu lilitikisa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani likiambatana na burudani kabambe kwa wasikilizaji wake kupitia masafa ya 93. 7 Efm.

Wakazi wa Bagamoyo walipata kushuhudia tamasha hilo lililofanyika katika Viwanja vya TOP TOP kwa kuhusisha vikundi mbalimbali vya jogging pamoja na kushiriki katika sakata la kumtafuta Bingwa wa Singeli Michano wa Wilaya hiyo.

Burudani hiyo ilisindikizwa na wasanii wa Singeli, Yuda Msaliti, Dogoo Niga na Khalid Chokoraa ikiambatana na Playlist kali ya Rdjs’ Mix ya Muziki iliyofanyika katika Ukumbi wa Mnene pale Mageti Mia.

Hadi sasa Tamasha la Muziki Mnene limeishafanyika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani ikiwemo Wilaya ya Mkuranga, Mlandizi, Kibaha na kwingineko.

Pia unaweza kuipata habari hii Youtube, tembelea sasa Global TV Online, au katika website yetu www.globaltvtz.com

Na Hilaly Daud/GPL

Comments are closed.