The House of Favourite Newspapers

Siri Dereva Wa MO Yafichuka

KUFUATIA sakata la kutekwa Mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘MO’, kuwa na maswali mengi juu ya uwepo wa dereva wake, hatimaye jibu limepatikana.

 

Mo alitekwa na watu wasiojulikana alfajiri ya juzi Alhamisi wakati akienda kufanya mazoezi kwenye Hoteli ya Collessium iliyopo Masaki jijini Dar.

Hata hivyo kumekuwa na maswali mengi kuhusiana na Mo kwa nini hakuwa na dereva wake huku wengi wao wakihoji alikuwa wapi, Championi Jumamosi limefanya uchunguzi na kupata ukweli wote.

Chanzo makini kilichozungumza na Championi Jumamosi, kimesema kuwa, siku hiyo yaani ile Alhamisi afrajiri dereva wake hakuambatana naye na alipanga akutane naye mara baada ya kumaliza mazoezi.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, huwa ni kawaida kwa Mo kwenda mazoezini peke yake na baada ya kumaliza hurejea nyumbani kujiandaa na baada ya hapo huongozana na dereva kwenda kwenye majukumu yake ya kila siku.

 

“Mara nyingi dereva wake huwa hawaambatani naye mazoezini labda kuwe na dharura na ndiyo maana siku hiyo ya kutekwa hakuwepo.

“Siku hiyo alitakiwa kukutana naye nyumbani ili waambatane pamoja kwenda kazini kama ambavyo hufanya siku zote lakini wakati anatoka kwake kuelekea huko ndiyo akasikia taarifa za kutekwa kwa bosi wake,” kilisema chanzo hicho na kuendelea kutiririka:

 

“Hakuziamini taarifa hizo hadi alipoamua kwenda moja kwa moja nyumbani kwake na kukuta ndugu na jamaa wamekusanyika ndiyo akajiridhisha.

“Jamaa anasema jana yake walitoka ofisini wakiwa na furaha tu, tena walipitia kwenye shughuli zake nje ya ofisi na baadaye akamrejesha kwake akiwa mwenye furaha tu.”

Stori: Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Comments are closed.