The House of Favourite Newspapers

Siri Jeuri ya Fedha ya Uwoya Yafichuka

KWA muda mrefu staa wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amekuwa akidaiwa kufanya kufuru ya fedha bila kujulikana chanzo cha mapato yake, lakini kupitia Ijumaa Wikienda siri nyuma ya jeuri yake ya fedha imefichuka.

 

Uwoya amekuwa akila bata kwenye viwanja vya gharama kubwa ikiwemo mahoteli makubwa huko Dubai, Zanzibar na mikoani hivyo kuibua maswali kwa mashabiki wake kuwa ni mapato ya filamu tu au?

Mbali na matanuzi na shopping za nguvu, Uwoya amekuwa akibadili magari makali huku akiendelea na ujenzi wa klabu yake ya gharama kubwa ya Last Minute iliyopo Sinza- Mori jijini Dar.

 

Kufuatia jeuri yake hiyo ya fedha, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Uwoya na ndipo akatoa siri nyuma ya kufuru zake.

Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Uwoya? Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni nani aliye nyuma ya jeuri yako ya fedha kwa sababu wanaamini msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz chende ‘Dogo Janja’ (anayesemekana ni mumewe) hana mkwanja huo?

Uwoya: Hakuna mtu, unajua sipendi kuweka mambo yangu hadharani. Haya ndiyo maisha yangu, ni kawaida.

Ijumaa Wikienda: Vitu kama safari za matanuzi nje na ndani ya nchi na shopping za kufa mtu ni nani aliye nyuma ya mambo haya?

Uwoya: Ni mimi tu nimeamua kupendeza. Kama ni kubadili nguo mimi nguo ninazo nyingi sana, sema zamani nilikuwa navaa, lakini sipigi picha. Nadhani hii ishu ya kuvaa na kuposti mtandaoni ndiyo inafanya watu waone ni nguo mpya.

 

Ijumaa Wikienda: Wengine wanadhani kwamba unatangaza nguo, lakini pia hujajibu ni nani aliye nyuma ya mambo hayo kwa maana ya mwanaume?

Uwoya: Mimi sitangazi nguo, ni nguo zangu huwa ninanunua kwa fedha zangu. Nimeamua tu kupendeza.

Kuhusu mtu mpya…hakuna, lakini kuna siri watu wengi hawaijui. Kwa sasa mambo yote yanasimamiwa na menejimenti yangu. Menejimenti ndiyo inanifanyia kila kitu ambacho watu wanaona ni jeuri ya fedha.

Ijumaa Wikienda: Watu wanasema kuna kipindi Dogo Janja alikuwa anaumwa kwa ajili ya penzi lako na wewe hukuonekana hospitalini ulikuwa unaendelea na bata zako, hilo vipi?

Uwoya: Wanasema anaumwa kwa ajili yangu? Basi hayo makubwa! Sijawahi kusikia kuna ugonjwa wa mapenzi. Kwa hiyo ina maana mimi huwa ninawatesa watu? Mimi huwa siteswi? Maana kila mtu Uwoya… Uwoya…ina maana kila ishu ya mapenzi mimi ndiye huwa natesa watu? Kwa hiyo mimi ni tesatesa au chinjachinja wa mapenzi? Ni kweli mimi ni mkali, lakini huyo mwanaume atakuwa na ugonjwa mwingine siyo mimi.

 

Ijumaa Wikienda: Lakini inasemekana umeachana na Dogo Janja, hili likoje?

Uwoya: No Coment! Kwani wakati tunaanza tuliwatangazia? Hilo waambie sina majibu, nimesema no coment!

STORI: Imelda Mtema, DAR

Comments are closed.