The House of Favourite Newspapers

Siri ya Chid Benz kupaka rangi nywele

RAPA mkongwe kunako Muziki wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro, ‘Chid Benz’ ametaja sababu ya kupaka nywele zake rangi kuwa, sio kama anawaigiza wasani wanaotoka Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) bali wakati wake umefika wa kubadilika kichwani.

 

Akizungumza na Star Showbiz muda mfupi baada ya kufika katika hafla aliyoiandaa msanii mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ juzikati ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa misaada eneo alilozaliwa (Tandale), Chid alisema;

 

“Unajua watu wanafikra tofauti na kupenda kuongea mambo mengi, mtu anapofanya kitu wanahisi tu atakuwa amewaiga watu wengine lakini mimi nimeamua kufanya hivi kwa kuwa wakati kwa upande wangu umefika,” alisema Chid Benz.

 

Chid pia alimgusia Diamond kwa kusema amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuufikisha Muziki wa Bongo Fleva mbali.

“Namuombea Diamond aendelee kupenda kazi yake kwani Muziki wa Bongo Fleva unafanya mengi mazuri tuu, kwa hatua alioifanya namuombea kwa Mungu azidi kufika mbali, mbali zaidi,” alimaliza Chid Benz.

Comments are closed.