The House of Favourite Newspapers

Siri ya Mahaba ya Sanchi na Mbwa!

JANE Rimoy ‘Sanchi’ ni mmoja wa wanamitindo Bongo ambao wameweza kujizolea umaarufu mkubwa kutokana na jinsi wanavyojiweka. Ni mdada aliyejipatia umaarufu kutokana na umbile lake na jinsi ambavyo amekuwa akipenda kupiga picha zake za kihasara hivyo kumfanya ajulikane sana ndani na nje ya Bongo.

Juzikati mwanadada huyu alizungumza na gazeti hili na kufunguka mambo mbalimbali ikiwemo mahaba yake kwa mbwa. Ili kujua alichoongea, fuatilia mahojiano hapa chini;

KUNA SIRI GANI KATI YAKE NA MBWA?

“Kiukweli napenda sana mbwa na mara nyingi nikiweka picha zangu nikiwa nimepozi na mbwa, mashabiki wangu wanaonekana kupenda sana. Likes na comments zinakuwa nyingi sana. Kwa kifupi nina mahaba makubwa kwa mbwa.”

Ni kweli anafanya biashara ya mbwa?

“Hapana, sifanyi biashara ya mbwa ila kupitia mapenzi yangu kwa mnyama huyo, nimepata dili la kuwa balozi wa mbwa aina ya Bull Dog.”

 

VIPI KUHUSU KUJICHANGANYA NA MASTAA WENZAKE?

“Yaani maisha haya mimi nayapenda sana kuliko chochote, mapenda kuwa peke yangu! Hii inanisaidia sana kuepukana na vitu vingi. Kuna umuhimu kweli wa kujichanganya na mastaa wenzangu lakini ni pale inapobidi.”

“Ninachofanya sasa hivi ni kuwa na marafiki wachache ambao watakuwa ni wenye faida kwangu kuliko kujichanganya na mastaa ambao mwisho wa siku najikuta kwenye maskendo yasiyo na maana.”

VITU GANI ANAFANYA 0

wa nikialikwa sana kwenye matamasha mbalimbali kuwa ‘host’. Kiukweli nimekuwa nikipata pesa nyingi kufuatia madili haya.

 

Nimekuwa nikiitwa kwenye shoo za hapa Bongo, Kenya, Uganda, Nigeria na kwingineko.”

VIPI HILI LA KUPOSTI PICHA ZA NUSU UTUPU?

“Unajua kuna mtu mwingine anaweza kudhani nafanya makusudi lakini ndiyo hobi yangu. Hata nguo ambazo navaa huwa ndiyo roho yangu inapenda nivae hivyo na siyo za nusu utupu kama watu wanavyosema.

“Na ukijaribu kunifuatilia utagundua kuwa nimebadilika sana kwenye suala la uvaaji kutokana na maneno ya watu.”

VIPI KUHUSU KUMILIKI MJENGO?

“Kwa hilo namshukuru Mungu, nimeweza kumiliki mjengo wangu wa maana kabisa na hivi karibuni nitauweka wazi maana niko kwenye hatua za mwishomwisho.”

Vipi kuhusu akaunti yake, inasomaje?

“Hayo mambo si unajua ni siri ya mtu. Ni ngumu sana kuyaweka wazi ila kaa ukijua niko makini sana kwenye mambo ya pesa. Si unajua tena Mchaga na pesa.”

KWA NINI HAPENDI KUMUWEKA WAZI MPENZI WAKE?

“Naona siyo sawa kabisa, kama ni wa kwangu kwa nini nimuanike? Sioni sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa nitamuanika leo nikiwa naye, kesho tukiachana tena niseme tumeachana kisha nimuanike mwingine, huo wala hauwezi kuwa mfumo sahihi wa maisha.”

NI KWELI ANAENDESHA MAISHA YAKE KWA KUTEGEMEA KALIO?

“Mimi namshukuru Mungu kwa kunipa umbo hili ambalo ni la asili kabisa. Hao wanaosema nategemea kalio kuendesha maisha yangu ni ‘mabogasi’. Akili yangu ndiyo inayoniongoza katika maisha yangu, kama ni shepu mbona wengi tu wana shepu lakini hawana mafanikio kama yangu?”

 

Na Imelda Mtema 

Comments are closed.