The House of Favourite Newspapers

Skaina anaswa akipiga ngumu kumeza

skaina-2 STORI: ANDREW CARLOS, IJUMAA WIKIENDA

DAR ES SALAAM: Ama kweli Januari ni mwezi dume! Staa wa sin­ema za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ juzikati amenaswa laivu ndani ya Klabu ya Maisha Basement, Kijiton­yama jijini Dar akinywa kilevi kikali ‘ngumu kumeza’ bila wasiwasi tofauti na alivyozoeleka kupiga vitu laini.

skaina-1Likiwa ndani ya kiota hi­cho cha burudani usiku wa manane, Wikienda lilimshuhudia Skaina akizama ukumbini hapo akiwa ameongozana na mashosti zake kwa ajili ya kula bata ndefu kama kawa­ida yao.

Wakati shoo ikiendelea, Skaina yeye alikuwa hana habari na mtu zaidi ya kuen­delea kushikilia glasi iliyokuwa na ngumu au konya huku akiinywa kana kwamba anaombea mwezi huu dume uishe tu kwa amani aanze kunywa vitu laini.

skaina-3Kuna muda alivamiwa na wen­zake mahali alipokaa kisha wakaanza kutandika ngumu kila mmoja huku kila mmoja akiupigia saluti Mwezi Janu­ari kwani mastaa wengi huwa wakienda maeneo ya starehe hupendelea kunywa vitu laini lakini sasa hivi ngumu kumeza ndiyo mpango mz­ima kwani inanyweka ki­dogo na kulewesha zaidi.

Wikienda lilimtimbia Skaina na kumuuliza kulikoni kunywa ngumu kumeza ambapo aliomba kuachwa kwani yupo kwenye starehe zake binafsi.

Comments are closed.